NEWS

19 Septemba 2018

BREAKING: CHADEMA WAJIONDOA RASMI CHAGUZI NDOGO ZOTE

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza kujiondoa Rasmi kushiriki chaguzi ndogo zote zilizotangazwa kufanyika hivi karibuni na chaguzi zozote zitakazofuata zinazosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa madai kwamba tume hiyo inafanya kazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe ameituhumu NEC akidai inafanya kazi ya kuhakikisha chama tawala chini ya Rais John Pombe Magufuli kinashinda kwa kulazimisha matokeo.

 

Mbowe amesema hawatashiriki katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Liwale na kata 37 kwa kile alichodai kuwa, kupitia maumivu mazingira magumu ya kisiasa na kiuchaguzi.

 

“Upole na ukimya wa vyama vya upinzani haushirii uoga hata kidogo, yale mawazo ya wenzetu wa Chama Cha Mapinduzi kuamini wana dola na ndio wenye nguvu ni kujidanganya, hakuna jeshi linaloweza kuwa na nguvu kuwazidi raia wa Tanzania,” amesema Mbowe.

The post BREAKING: CHADEMA WAJIONDOA RASMI CHAGUZI NDOGO ZOTE appeared first on Global Publishers.