
KIVUKO cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorara na Kisiwa cha Ukala katika ziwa Victoria (wilayani Ukerewe mkoani Mwanza) kimezama huku taarifa za idadi ya watu waliokuwemo ndani ya kivuko hazijajulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara na kwamba kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa 8:00 mchana kilipinduka.

Aidha, Shana amesema bado hawajapata idadi kamili ya waliokuwemo kwenye kivuko hicho. Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho na yuko njiani kulekea huko na watatoa taarifa baadaye.
The post Breaking: Wahofiwa Kufa Maji Baada ya Kivuko Kuzama Mwanza appeared first on Global Publishers.