NEWS

20 Septemba 2018

GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI LATINGA MTAANI

TIMU nzima ya wafanyakazi wa Global Publishers, wakiongozwa na Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho, mapema leo wametinga mtaani kulinadi gazeti la Spoti Xtra ambalo ni jipya na ambalo limekuwa likiingia mtaani siku za Jumaili  na sasa limeanza kuingia mtaani kila siku ya Alhamisi kwa bei ya shilingi 500.

Akizungumzia ujio huo wa gazeti hilo la Spoti Xtra kila Alhamisi, Mrisho amesema lengo kubwa ni kumaliza kiu ya wapenzi wa habari za michezo na ndiyo sababu kubwa ya kuliingiza mtaani siku hiyo.

Wasomaji wa gazeti la Spoti Xtra ambao walichangamka kulinunua maeneo ya Stendi ya Makumbusho na maeneo ya makutano ya mataa ya Morocco-Kinondoni, wamelipongeza kwa mwonekano mzuri na kwa namna ambavyo limesheheni habari za michezo.

“Kiukweli nyie watu wa Global mmetusaidia sana kuliingiza gazeti hilo siku ya Alhamisi kwani tumekuwa tukikosa habari za michezo na kubaki tukitafakari nini cha kufanya, hongereni sana,” alisema  mmoja wa madereva wa stendi ya makumbusho aliyejitambulisha kwa jina la Masudi Khamis.

The post GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI LATINGA MTAANI appeared first on Global Publishers.