NEWS

21 Septemba 2018

MV NYERERE: PICHA 9 KUTOKA ENEO LA TUKIO, HALI ILIVYO

MAJONZI MAZITO! Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwelwe amesema uokoaji wa miili ya waliofariki dunia baada ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere utakamilika leo Septemba 21, 2018 kabla ya saa 12 jioni huku lengo likiwa ni kuhakikisha wanawaokoa wote walionasa kwenye kivuko hicho.

Kamwelwe ametoa kauli hiyo leo mchana wakati akihojiwa na kituo cha Utangazaji cha Taifa (TBC), akiwa eneo la tukio Kisiwa cha Ukara wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.

Mpaka sasa miili zaidi ya 100 imepatikana katika ajali hiyo kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

The post MV NYERERE: PICHA 9 KUTOKA ENEO LA TUKIO, HALI ILIVYO appeared first on Global Publishers.