NEWS

23 Septemba 2018

Updates: Waziri Kamwele Asema Waliofariki Dunia Kivuko cha MV Nyerere ni 224 Hadi Mchana huu

Waziri Uchukuzi, Isack Kamwelwe amesema kivuko cha MV Nyerere kilikuwa kimebeba watu 265 tofauti na uwezo wake wa kubeba watu 101.
   
Kawele ametoa kauli hiyo leo Jumapili Septemba 23, 2018  wakati wa ibada ya Mazishi ya miili ambayo haijatambuliwa na ndugu zao.

Amesema idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia ajali hiyo  iliyotokea Ukara Wilayani Ukerewe imefikia 224.