Msanii wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu leo baada ya kuitwa kuhojiwa na Bodi ya Filamu Tanzania kuhusu kusambaa kwa picha na video zake chafu kwenye mitandao ya kijamii, imeamua kumfungia msanii huyo kujishughulisha na mambo ya filamu.
Bodi hiyo imeamua kumfungia msanii huyo na kumtaka kutojishughulisha na filamu kwa muda usiojulikana, kufuatia picha zake chafu zilizosambaa mtandaoni.
Ikubukwe kwamba jana October 25, msanii huyo aliomba msamaha kutokana na tukio hilo ambalo lilitokea siku kadhaa nyuma ambapo alionekana akiliwa denda na mwanaume anayesemekana ni raia wa Burundi.
Hata hivyo, Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza akizungumzia juu ya msamaha huo amesema kuwa ni unafiki mkubwa kwani sio mara ya kwanza wala ya pili kwake.
“Hii ni kama unafiki fulani, kwa sababu hii sio mara ya kwanza kwa msanii huyu, wala sio mara ya pili, na niseme tu kwamba kwa upande wa Baraza lina mchango wake kufikia hapo alipofikia, ile ni unafiki, haitoshi, mtu mara ya kwanza ya pili unasema hii ni tabia zake, na kwa vile kuna sheria zingine zilizovunjwa, lazima wahusika wachukue hatua zake, hii haitoshi, lazima awe mfano”, amesema

Wema amekuwa akijihusisha mara kwa mara na matukio ya kusambaza picha zisizo na maadili mitandaoni na amekuwa akionywa na vyombo husika lakini mara hii vimeamua kumfungia kabisa kutojihusisha na mambo ya filamu.