BUNGE la Ethiopia limemchagua Sahle-Work Zewde kuwa rais wa kwanza mwanamke wa nchi hiyo. Sahle-Work ni mwanadiplomasia mkongwe ambaye anakuwa mwanamke wa kwanza kuwa mkuu wa nchi barani Afrika.
Kuchaguliwa kwake kunakuja baada ya wiki moja ambapo Waziri Mkuu, Abiy Ahmed, ameteua nusu ya baraza lake la mawaziri wanawake.
Kushika kwake nafasi hiyo kumepokelewa kwa furaha na mitandao ya kijamii ya Ethiopia ikisema ni kitendo cha kihistoria, kinachokumbusha enzi za Malkia Zewditu aliyeiongoza nchi hiyo mwanzoni mwa karne ya 20.
Mbali na kushika nyadhifa kubwa kama msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rais Sahle-Work pia ameiwakilisha Ethiopia kama balozi katika nchi za Senegal na Djibouti, alikuwa pia mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika Umoja wa Afrika (AU).
The post Sahle-Work Zewde Awa Rais wa Kwanza Mwanamke Ethiopia appeared first on Global Publishers.