NEWS

15 Desemba 2018

KOCHA YANGA AMKATAA BENO, ASEMA ATAFUTIWE TIMU

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera.

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, amekataa kumpokea kipa wake Beno Kakolanya baada ya kugomea kuitumikia timu yake kutokana na madai ya kutolipwa stahiki zake.

 

Hivi karibuni Kakolanya aligoma kuitumikia Yanga akishinikiza kulipwa fedha zake za usajili pamoja na mshahara wa miezi kadhaa ambao hajapata mpaka sasa.

 

 

Maamuzi hayo ya Kakolanya kugoma yalifanya Zahera aibuke kupitia vyombo vya habari na kuelezwa kushangazwa naye mpaka imefikia hatua ya kutomhitaji tena katika kikosi chake.

 

Aidha, Zahera ameongeza kwa kumtaka mchezaji huyo ni vema akatafutiwa timu nyingine kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa kesho saa 6 kamili usiku kwa maana yeye hamhitaji tena.

“beno hawezi tena kurudi kwenye timu, walimwambia asije mazoezini hivyo wanapaswa kumtafutia timu nyingine, ila hapa kwetu nadhani haitawezekana tena” amesema.

 

Inaelezwa Kakolanya anaidai Yanga kiasi cha shilingi za kitanzania, milioni 15 kama fedha ya usajili pekee ukiachana na zile za mshahara.

The post KOCHA YANGA AMKATAA BENO, ASEMA ATAFUTIWE TIMU appeared first on Global Publishers.