NEWS

31 Agosti 2019

Mwanamke Mshona Viatu Aliyejenga Nyumba, Asimulia Mazito Aliyopitia – Video

Ingawa Dunia ya Sasa Wanawake wengi wamejikuta wakihamasishana kuwa na haki sawa na Wanaume, lakini bado Kuna kazi nyingi zinazofanywa na Wanaume ambazo Mwanamke akionekana anazifanya huonekana wa tofauti kwenye jamii.

Mwanadada anaetambulika kwa majina ya Bupe Mwaipopo ambaye ameendelea kuwa gumzo Maeneo ya Ubungo Jijini Dar es salaam kwa kuamua kuwa Fundi Mshona Viatu (Shoe Shiner) licha ya kuwa Mrembo na mwenye umbo la kuvutia amejikuta akidhiirisha ule usemi usemao kuwa Ukistaajabu ya Musa basi utayaona ya filauni.

Global tv, tumeamua kufatilia mpaka eneo lake la kazi na kuzungumza nae kuhusu Historia ya Maisha yake, changamoto na sababu kubwa iliompelekea kuamua kufanya kazi hio sanjari na kuzungumza na Baadhi ya wateja wake wa eneo hilo.

The post Mwanamke Mshona Viatu Aliyejenga Nyumba, Asimulia Mazito Aliyopitia – Video appeared first on Global Publishers.