NEWS

28 Septemba 2019

Wanaume Wanavyolizwa Magroup ya WhatsApp

WIKI iliyopita sehemu ya kwanza ya ripoti hii ilieleza jinsi ambavyo wanaume wakware wanaopenda ngono na kuchepuka wanavyolizwa kupitia ‘ma-group’ (makundi) ya ngono ya WhatsApp ambayo sasa yamesambaa kwenye mitandao ya kijamii.

 

Inaelezwa kwamba, mchezo mzima huanzia Mitandao ya Facebook na Instagram ambapo wengi wa matapeli hao huweka picha za wanawake wazuri wa sura na wenye shepu matata wa Kibongo na kudanganya kuwa wanapatikana kwa njia ya picha na video wakiwa utupu kwenye makundi yao ya WhatsApp huku wakianika namba za simu watumiwe kiasi cha pesa waunganishwe, sasa endelea.

 

Uchunguzi wa Gazeti la Ijumaa ulibaini kwamba, kuna visa vingi vya wanaume ambao wamelizwa kupitia makundi ya WhatsApp, lakini wamekuwa wakificha ili kutoonekana wajinga.

 

Ilibainika kuwa, katika mitandao ya kijamii kuna biashara ya ngono ambayo sasa imeshamiri na inakuwa kwa kasi ya ajabu na bila kificho kama mwanzo.

Kama wewe ni mtumiaji wa Mtandao wa Facebook kwa sasa kuna kurasa nyingi mno zinazojishughulisha na matangazo ya biashara hii haramu inayokwenda kinyume na maadili ya Kitanzania.

 

Ili kutozipa umaarufu kurasa hizo, ni busara kutozitaja, lakini Gazeti la Ijumaa limeshuhudia kurasa ‘pages’ ya zaidi ya 100 ambazo watu wengi ‘wamezishea’ wengine kwa kujua na wengine kutokujua.

Kurasa hizo zimekuwa zikielekeza watu kujiunga kwenye makundi ya WhatsApp kwa kutoa namba za simu za za mitandao mbalimbali kwa ajili ya mtu kujiunga.

 

Kurasa hizo huambatanishwa na picha au video za utupu au nusu utupu zenye lengo la kuibua hisia za ngono kwa wanaume.

Matangazo ya makundi haya ya WhatsApp huambatana na picha ya ngono ya mwanamke na ujumbe f’lani unaosomeka;

 

“Nina hamu na mume wa mtu, kama umenipenda nitafute kwenye group la WhatsApp namba…..”

Ndani ya makundi hayo ya WhatsApp, mtu ambaye hujifanya mwanamke kwa kutumia picha ngono za wanawake weusi wanaoigiza filamu za ngono duniani, huanza kuchati na mwanaume anayeingia mkenge kisha humtumia picha za utupu na kuomba kuonana ili kufanya ngono.

 

Hata hivyo, uchunguzi wa Ijumaa umejiridhisha kuwa ahadi hizo za kukutana huwa hazitimii badala yake mwanaume hujikuta akipewa matumaini na kuomba kutuma pesa kila kukicha.

 

Mwingine humtumia mwanaume picha zake za utupu kisha kuomba vocha au nauli ili wakutane na baada ya kudaka mshiko wa mwanaume huyo asiyejua kuwa anaibiwa huingia mitini na namba inakuwa haipatikani.

Kwenye magroup hayo akina dada hufundishana umalaya na namna ya kuwaibia waume za watu.

 

SERIKALI INASEMAJE?

Joshua Mwangasa ni Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini kutoka kitengo cha uhalifu wa mtandao (cyber crime) katika makao makuu ya polisi jijini Dar ambaye anasema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kuwabaini wale wote wanaoendesha biashara ya kujiuza na kuweka picha za uchi kwenye mitandao ya kijamii hususan kwenye Whatsapp na Instagram.

 

Kamanda Mwangasa anasema kwamba, tayari watu kadhaa walishashikiliwa ili kuhakikisha kuwa wanawabaini wote, kwani kujiuza na kuweka picha za utupu kwenye mitandao ikiwemo WhatsApp ni kosa la jinai kupitia Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.

 

Kamanda Mwangasa anasema, sheria hiyo pia inapiga marufuku mtu yeyote kuweka mtandaoni video au picha inayoonesha mambo ya kingono au ukatili wa kingono kwa watoto, hivyo yeyote atakayetenda makosa hayo na kubainika mara moja atashikiliwa na jeshi hilo.

 

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza anatoa onyo kwa wasanii nchini kuacha kutumia vibaya mitandao ya kijamii na endapo hawatafanya hivyo, basi watachukuliwa sheria stahiki dhidi yao.

Stori: WAANDISHI WETU,Ijumaa

-MWISHO-

The post Wanaume Wanavyolizwa Magroup ya WhatsApp appeared first on Global Publishers.