NEWS

28 Septemba 2019

Zabibu: Siwezi Kuingilia Ndoa za Kaka Zangu

UKISIKIA mawifi ambao hawataki shobo ndiyo kama huyu dada wa mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Ally Saleh Kiba ‘AliKiba’, Zabibu Kiba ambaye ameweka wazi kamwe hawezi kuingilia ndoa za kaka zake.



Zabibu alitoa kauli hiyo juzikati alipoulizwa na Showbiz Xtra kuhusu ndoa za kaka zake, Kiba na Abdu ambazo zinaonekana kupumulia mashine.



“Unajua siyo kitu kizuri kabisa kuingilia ndoa za kaka zako, ninachojua wale ni wifi zangu kama huko nyuma nilivyotambulishwa na siyo hivyo tu tulicheza na harusi sasa ikifika wakati kama ndoa zao hazipo wataniweka wazi kama dada lakini kwa sasa bado sijaambiwa chochote kile na pia nawaombea ndoa zao ziendelee kudumu,” alisema Zabibu.