Wahamiaji haramu 41 kutoka nchini Afghanistani wakamatwa katika lori la kusafirishia samaki na nyama nchini Ugiriki.
Miongoni mwa wahamiaji hao waliokamatwa 7 walipelekwa hospitali kupatiwa matibabu kutokana na hali waliokuwa nayo kutokana na uhaba wa hewa safi katika lori hilo.
Wahamiaji hao wamekamatwa Jumatatu wakiwa na dereva wao kama ilivyofahamishwa na jeshi la Polisi.
Lori hilo lilifanyiwa uchunguzi na Polisi kati ya mji wa Xanthi na Komotini Egnatia.
Dereva wa gari hilo ni raia kutoka nchini Georgia, amewekwa chini ya ulinzi.
Jeshi la Polisi limefahamisha kumsaka mtu mwingine kutoka Uturuki ambae anashukiwa pia kuhusu na usafirishaji haramu wa binadamu.
Tukio hilo limetokea baada ya tukio kama hilo kutokea nchini Uingereza ambapo raia 39 ambao walitajwa kutoka Vietnam walikutwa wamefariki.
Ugiriki imekumbwa na wimbi kubwa la wahamiaji kutokana na kutokuafikiana na Uturuki kuhusu suala la wahamiaji tangu mwaka 2016.