NEWS

31 Januari 2020

Salama Jabir Atoa Tahadhari hii


Mtangazaji maarufu nchini Tanzania Salama Jabir, amesema ujio wa kipindi chake kipya cha SalamaNa, hakitakuwa na watu mastaa peke yao bali mtu yeyote mwenye stori nzuri, pia ametaka shughuli zake zisifananishwe na watu wengine.


Akiongea mbele ya waandishi wa habari ambao walijitokeza katika uzinduzi wa kipindi chake, Salama Jabir amesema anataka vitu vya kipekee na tofauti, kwa sababu anafanya kazi na watu walio bora kabisa.

"Kipindi changu sio lazima wawe watu maarufu tu, anaweza akawa hata mtu mwingine kama ana stori nzuri tunamsikiliza, halafu tunafanya naye, shughuli zangu zinajulikana, tafadhali msizifananishe na mtu yeyote, mimi nataka vitu vya kipekee na tofauti kwa sababu nafanya kazi na watu walio bora sokoni pia hatutaki kufanya vitu ambavyo wengine wanafanya na hilo suala tunalikwepa kila siku" ameeleza Salama Jabir.

Kipindi cha SalamaNa kitakuwa kinaruka kila siku ya Alhamisi kuanzia 3:00 usiku, kupitia East Africa TV.

Baadhi ya watu ambao ameshafanya nao katika kipindi hicho ni  Lil Ommy, Marco chali, Jokate Mwegelo, Barnaba Classic, Shilole, Mx Carter, Fid Q, Idriss Sultan, Khadija Kopa, Mwana Fa , Ben Pol na Gigy Money.