Hili ni moja ya Matukio yanayozungumziwa zaidi Mitandaoni na kuchagiza hoja ya Ubaguzi wa rangi unaoendelea nchini Marekani kwasasa
Huyu ni Sebastian Arzadon , Aliyekamatwa juzi kwa kesi ya Mauaji ya watu wawili huko Lawrenceburg nchini Marekani. Licha ya kuwa ni muuaji , Sebastian alikamatwa vizuri na polisi ikiwemo kumpatia maji ya kunywa pamoja na kumsafisha majeraha yake kabla ya kumpeleka kituoni
Hali ni tofauti kwa Wamarekani weusi , ambao wengi wao huteswa na polisi ikiwemo kupigwa risasi , kwa makosa yasiyo na uzito , na polisi wanaofanya hivyo kutochukuliwa hatua yoyote
