NEWS

8 Septemba 2020

Mahakama ya Saudi Arabia yawapungunzia adhabu waliomuua Jamal Khashoggi



Waendesha mashitaka wamesema kuwa walipewa hukumu ya miaka 20 jela baada ya baada ya familia ya Khashogi ambaye alikuwa ni mwaandishi wa habari kuamua kuwasamehe
Mahakama nchini Saudi Arabia imeondoa hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya watu watano waliopatikana na hatia ya mauaji ya Jamal Khashoggi, mwaka 2018, vimesema vyombo vya habari.

Waendesha mashitaka wamesema kuwa walipewa hukumu ya miaka 20 jela baada ya familia ya Khashoggi ambaye alikuwa ni mwaandishi wa habari kuamua kuwasamehe.

Hatahivyo, mchumba wake amesema uamuzi uliofanywa ni "ni kejeli ya haki kabisa''

Khashoggi, ambaye alikuwa mkosoaji maarufu wa serikali ya Saudia aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Ufalme wa Saudia katika mji mkuu wa Uturuki Instanbul na maafisa wa ujasusi wa Saudi Arabia.

Serikali ya Saudia ilisema kuwa mwandishi huyo wa habari aliuawa katika "operesheni ambayo haikukusudiwa " na mwaka uliofuatia Saudi Arabia iliwashitaki watu 11 mahakamani kuhusiana na kifo hicho.