NEWS

25 Septemba 2020

Polepole: Wapinzani Waungane Tutawachapa Asubuhi



KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole,  leo Septemba 25, 2020, amesema chama chake kitavishinda vyama vyovyote vya upinzani vitakavyoungana katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Ameyasema hayo wakati akitoa tathmini ya kampeni za uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho.

“Mimi natoa rai wasisubiri Oktoba 3, 2020, ili waungane, hawa waungane sasa halafu ndiyo watajua tulipotoka na tulipofika na Watanzania. Sisi tumeingia nchi hii ikiwa ni maskini huyu Mzee Magufuli kapambana leo sisi ni nchi ya uchumi wa kati,” amesema.

Aidha aliwashutumu wapinzani  kwa kile alichodai kutumia uongo kwenye kampeni zao.

“Wenzetu wa upinzani wamekuwa mstari wa mbele kutumia uongo kama nyenzo ya kampeni, uongo mkubwa, upotoshaji wa makusudi, na uzuri Watanzania waunajua uongo watu hawa wanaousema.”