Machinga wa jijini Dar es Salaam wameungana na kutoa tamko la kupinga maandamano yaliyotangazwa na viongozi wa Chadema na ACT Wazalendo.
Wamachinga hao wamempongeza Rais Magufuli kwa ushindi katika uchaguzi mkuu na kusema watakuwa naye bega kwa bega kwani ni muokozi wa wanyonge.