NEWS

17 Desemba 2020

Jumla ya wanafunzi 759,706 Wachaguliwa Kujiunga kidato cha kwanza 2021


Jumla ya wanafunzi 759,706 sawa asilimia 91.1 kati ya wanafunzi 759,737 waliokuwa na sifa za kujiunga na kidato cha kwanza, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021.

Uchaguzi huo umetangazwa leo Alhamis Desemba 17, 2020 na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo.

Amesema kati ya idadi ya waliochaguliwa 368,174 ni wavulama na wasichana ni 391,532.

Amesema kati ya waliochaguliwa wanafunzi 4,169 wamechaguliwa kujiunga na shule za bweni, ambapo wanafunzi 970 watajiunga na shule za wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi.

Hata hivyo, Jafo amesema jumla ya wanafunzi 74,166 sawa na asilimia 8.9 wakiwamo wavulana 34,861 na wasichana 39,305 hawakupangiwa shule katika awamu ya kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.

Jafo amesema  mikoa tisa ya Kagera, Katavi, Lindi, Mtwara, Mwanza, Njombe, Ruvuma, Songwe na Tabora imefanikiwa  kuwapangia shule wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza.