NEWS

11 Januari 2021

Rais Mwinyi Aifungua Skuli Ya Sekondari Ya Hasnuu Makame....Awataka Wanafunzi Kusoma Kwa Bidii Na Nidhamu


 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka wanafunzi kutumia vyema fursa za kuwepo miundombinu bora ya masomo  kwa kusoma kwa bidii na nidhamu.


Dk. Mwinyi amesema hayo  katika Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame , iliopo Kibuteni Mkoa Kusini Unguja.


Amesema wanafunzi watakaopata nafasi ya kusoma katika skuli hiyo wanapaswa kutumia vyema fursa hiyo kwa kusoma kwa bidii, ili waweze kufaulu katika amsomo yao badala ya  kujihusisha na masuala yatakayosababisha kuharibikiwa katika maisha yao ya baadae.


Alisema ni matumaini yake kuwa wanafunzi watakaosoma skuli hiyo watafulu vyema katika mitihani yao ya Taifa, kw akuwa   skuli hiyo iko katika mazingira mazuri, walimu wazuri pamoja na kuwa na vifaa vya kutosha.


Aidha, aliwataka wakuu wa Wilaya na mikoa kushirikiana na wananchi ili kufanikisha wanafunzi wote watakaotoka katika skuli 34 za Sekondari mkoani humona kujiunga katika Skuli hiyo wanafaulu vizuri.


Vile vile aliwataka walimu kutekeleza ipasavyo wajibu wao wa kusomesha vizuri pamoja na wazazi na walezi kufuatilia maendeleo ya elimu ya watoto wao ili kubaini chanagmoto zinazoweza kujitokeza.