NEWS

23 Agosti 2021

Taarifa ya TCU: Waombaji 68,019 Wachaguliwa Kujiunga Vyuo Mbalimbali Awamu ya Kwanza, Dirisha Awamu ya Pili Kufunguliwa Kesho


Waombaji  68,019  sawa na asilimia 73.2 ya waombaji  92,809, wamechaguliwa kujiunga katika Taasisi za Elimu ya Juu kwa kozi za Shahada za kwanza kwa mwaka wa masomo 2021/2022.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Tanzania (TCU) Profesa Charles Kihampa amesema ongezeko la waombaji limetokana na kuongezeka kwa wahitimu wa kidato cha sita.

Aidha Profesa Kihampa amesema dirisha la awamu ya pili la udahili linafunguliwa kesho Agosti 24,2021 mwaka huu hadi Septemba 6 mwaka huu, ili kutoa fursa kwa waombaji waliokosa nafasi kuomba katika awamu hiyo.

TCU imewataka waombaji kutuma maombi moja kwa moja katika vyuo, na kwa waombaji 35,548 waliochaguliwa chuo zaidi ya kimoja katika awamu ya kwanza ya udahili wanatakiwa kuthibitisha chuo kimojawapo katika vile walivyochaguliwa.

 

==>>Kuona Majina ya Waliochaguliwa chuo zaidi ya Kimoja ,BOFYA HAPA