Samirah Yusuph,
Maswa. Shirika la world vision Tanzania limefunga mradi wa maendeleo ya jamii katika jamii ya Isanga wilayani Maswa Mkoa wa Simiyu na kuukabidhi mradi huo kwa serikali.
Mradi huo ulioanzishwa mwaka 2016 ukilenga kuisaidia jamii ya kijiji cha Isanga katika nyanja za elimu, afya, maji na usafi wa mazingira, kilimo pamoja na ulinzi wa mtoto.
Ambapo umefanya utekelezaji wa shughuli zake katika vijiji 22 vya wilaya ya Maswa na kuwafikia jumla ya walengwa 71,815.
Akizungumza katika hafla ya kufunga mradi huo mwenyekiti wa jamii ya Isanga amesema mafanikio yaliyo patikana kwa kipindi cha miaka 15 ya utekelezaji wa mradi ni pamoja na kuwafikia wakulima 1959.
Ambao wamepewa mafunzo ya kilimo bora, kilimo cha umwagiliaji uzalishaji wa chakula lishe, ufugaji wa nyuki, na ufugaji wa kuku pamoja na kuwapa mafunzo maafisa ugani 19 na kuchimba mabwawa 109 na kutoa pampu 10 za umwagiliaji.
"Katika afya wanawake zaidi ya 1000 wamepewa mafunzo ya kuandaa chakula lishe ili kukabiliana na tatizo la udumavu kwa watoto pamoja na kutoa mafunzo kwa kamati za shule 21 kuhusu usimamizi na udhibiti wa ubora wa elimu," alisema Kombe.
Akisoma salamu za mfadhiri kutoka uholanzi Meneja wa world vision kituo cha Kanadi Ngassa Michael alisema kuwa ni furahakuona watoto na familia zao wanaweza kupata maji safi, afya zimeboreka nabmagonjwa kama kuhara yamepungua.
Aidha Mkurugenzi wa world vision Tanzania Nesserian Mollel ameishukuru jamii ya watu wa Isanga kwa ushirikiano walioonyesha hasa katika ufadhiri wa watoto kufuatilia na kushiriki vilivyo kwenye shughuli za mradi.
" Muda wa utekelezaji wa shughuli za mradi umeisha tumeiachia serikaki na wadau wengine katika jamii, kupitia mradi huu ipo miradi mingi imetekelezwa na jamii inanufaika lengo likiwa ni kutatua changamoto na mambo mengine katika nyaja za kijamii".
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila amepokea mradi huo na kupitisha ombi la wanajamii wa Isanga wa kuyafanya majengo yaliyotumika kama ofisi za mradi kuyageuza kuwa zahanati ili wanajamii wapate huduma za afya.
Mwisho.