“Sina cha kusema muziki unalipa, nyumba yangu ni kubwa sana na pia nimejaribu kuonyesha ni mafanikio gani ambayo nimeyapata mpaka sasa. Kwahiyo namshukuru Mungu na mashabiki ambao wananiwezesha,” amesema Mavoko.
“Wapo ambao walipata bahati kama yangu wakashindwa kuitumia, kwa mimi nimetumia nafasi niliyoipata, ndio maana nafanya mambo makubwa kama ninavyoingia gharama ya laki 8 kwajili ya mavazi kwenye shoo zangu kubwa. Kila show kubwa natoa laki 8 kwa mbunifu wangu.”
Aliongeza kuwa muziki hauna bahati bali ni kujituma.
