Babu Seya na Papii Kocha walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi watoto wa shule ya Msingi, Mashujaa, Sinza jijini Dar es Salaam.
Wawili hao wamewahi kukata rufaa tena na hawakufanikiwa na hukumu hii ya rufaa ni ya mwisho kusikilizwa. Katika rufaa hiyo wakili wa Babu Seya na Papii Kocha alikuwa akiiomba mahakama hiyo ifute ushahidi na waachiwe huru.
