Angel na Jennifer baada ya kuambiwa wameyaaga mashindanoJumamosi hii walimu wa academy wamefanya mabadiliko ya kushtukiza ambapo washiriki hawakutakiwa kumwokoa mshiriki mwenzao na hivyo kuwafanya Angel na Jennifer wote kwa pamoja kuondoka.
Fess ndiye mshiriki aliyepata kura nyingi na huku Phionah wa Rwanda akiokolewa na majaji.
Kuondoka kwa Angel aliyekuwa akitegemewa sana mwaka huu kunafanya Tanzania imebakize mshiriki mmoja tu, Hisia na kuendelezea utamaduni wa waimbaji wa Tanzania kutolewa mapema kwenye shindano hilo.