
Video hiyo itafanywa na kampuni ya Ogopa Videos ya Kenya.
Akiongea na ‘Chumba Cha Sindano’ kupitia kipindi cha Kali za Bomba cha Bomba FM Mbeya, Bob Junior aliongeza kuwa Bashasha imepokelewa vizuri kuliko ngoma zake zote toka kuanza kwake muziki.
“Safari hii miguu ya shingo tu kwa kila mtu. Video tuna-shoot Jumatano inayofuata yah!, lakini ni nyimbo ambayo kwakweli toka nimeanza muziki hii ni nyimbo ambayo umepokelewa kwa nguvu sana sijawahi kuona,” alisema.
“Mazingira ya video ni mazingira ni makubwa kwakweli. Tumeandaa dola elfu 10, kwaajili ya video ya bajeti hiyo sijui sasa kama itamalizika, itaisha lakini bajeti ipo tu imewekwa milioni 16 ya kibongo.”
By Greyson Chris Bee (Bomba FM)