Belle,amesema muziki wa sasa unabadilika hali iliyomfanya afikirie kuongeza nguvu kwa kumshirikisha Wyre.
“Nimekuwa nafanya muziki wangu kiubunifu sana. Ukiangalia nyimbo zangu zote zipo tofauti tofauti sana,ukianzia na wimbo wa Masogange,Nilipe Nisepe na Listen, zina utofauti sana. Hali hii inatoka na kuangalia Watanzania wanataka nini ndio maana hata sasa hivi nimeamua kufanya wimbo na Wyre wa Kenya na producer atakuwa Sappy yule aliyofanya wimbo wa Prezzo ‘Celebration of Life’, Alisema Belle.
Sappy ni producer wa Tanzania anayefanya kazi kwenye studio za Homeboyz Production na ndiye aliyetengeneza hit ya Redsan, Badder Than Most.