Kanye ambaye kichwa chake hivi sasa kinawaza zaidi mambo ya fashion, anaichukia kampuni ya Nike kwa kile anachodai kushindwa kumlipa mirahaba baada ya mauzo ya Air Yeezy trainers.
Muda mfupi baada ya Kanye kuwatosa Nike na kupata deal mpya na kampuni nyingine ya Adidas, rapper wa Canada Drake aliziba nafasi yake kwa kusaini dili na kampuni hiyo ya Nike.
Kwa mujibu wa TMZ, Kanye amefurahishwa na fursa aliyopata Drake kuziba nafasi yake kwa Nike, lakini bado anaichukia Nike kwa kumchukulia poa.
Wiki iliyopita Adidas walithibitisha rasmi kuingia mkataba na Kanye, ambayo ni dili ya $10 million.

