Ina buttons zinazoweza kutumika kupokea simu, na kuplay muziki uliopo katika smartphone ya mtumiaji.
LED screen ya pete hiyo huwaka pindi mtu aliyeivaa anapopokea e-mail, ujumbe mfupi, facebook na twitter notification, au simu inapoingia, na pete hiyo inaweza pia kutumika kama remote control.
Smarty Ring imebuniwa na engineer Ashok Kumar kutoka Chennai, India.
Pete hiyo imetengenezwa na ‘Bluetooth 4.0 sensor’ inayoweza kuunganishwa na simu yoyote ya Android au iOS kupitia application maalum ya Smarty Ring.
Simu inapoingia, aliyeivaa pete anauwezo wa kuchagua kupokea au kuikata simu kwa kutumia buttons ambazo ziko pembeni mwa pete hiyo.
Mwezi September wabunifu wengine wa Hungary walitambulisha pete kama hiyo ‘Ring Clock’, ambayo yenyewe inaonesha muda pekeyake.
SOURCE: MAIL ONLINE


