NEWS

16 Januari 2014

B12 , Adam Mchomvu na Diva Watimuliwa Clouds FM

Clouds Fm imeamua kuchukua maamuzi magumu ya kuwasimamisha kazi kwa muda usiofahamika watangazaji wake maarufu yaani Hamis Mandi ‘B 12’, Adam Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva’ .



 Kwa mujibu wa gazeti la Risasi Mchanganyiko zinasema kuwa uongozi wa Clouds umefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na tabia ya utovu wa nidhamu wa watangazaji hao. “Ni kweli tumefikia uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na Mchomvu baada ya kukiuka baadhi ya makubaliano baina yao na ofisi hivyo kusababisha usumbufu mkubwa ambao ulitulazimu kuingia gharama ambazo hazikutarajiwa” alisema mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa clouds Media Ruge Mutahaba.

“Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana ingawa watu wengi wamekuwa wakinihoji juu ya hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza watu wake, sasa hao wamevunja taratibu zetu,” Aliongezea Bwana Ruge Mutahaba.

Alipoulizwa ni taratibu zipi watangazaji hao walizovunja alisema: “Nashindwa kueleza kosa la kila mmoja ila naomba nieleweke kuwa hao watangazaji kwa sasa tumewasimamisha kwa muda usiojulikana wakati tukifikiria cha kufanya. Muhimu hapo ni kwamba wamekwenda kinyume na tulivyokubaliana.”