Akizungumza wikiendi iliyopita nyumbani kwake, Kimara - Temboni, Dar, mama huyo alisema, kama mwanaye angekuwa hai angekuwa amepata mke bora wa maisha yake, naye pia alikuwa na mkwe sahihi.
“Najua mtoto wangu ametangulia mbele za haki lakini faraja anayonipa Lulu ni kubwa mno na najisikia furaha. Kama Mungu angemwacha Kanumba hai mpaka leo kwa kweli Lulu angekuwa mkwe bora sana kwangu.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
“Sina jinsi, ndiyo imeshatokea lakini mimi kama mzazi bado nitaendelea kumpenda na kuwa bega kwa bega na Lulu hata akipata mchumba mwema wa kumuoa, sina tatizo na hilo... namwombea sana kwa Mungu huyu binti,” alisema kwa hisia mama Kanumba.

Source: Global Publishers