Marafiki na familia ya Nyong’o ambaye ni Mkenya aliyezaliwa Mexico huku wazazi wake wote wakiwa ni Wakenya, wamemfanyia misa hiyo Jumapili iliyopita katika kanisa la Ridgeways Baptist.
Hii ilikuwa pia ni njia mojawapo ya kushehereka mafanikio yake ya Hollywood ambapo amefanikiwa kunyakua tuzo kadhaa kutokana na ushiriki wake mzuri katika filamu ya ‘12 Year A Slave’.
Lupita amekuwa akipata support pia ya baba yake mzazi Anyang Nyong’o ambaye ni Seneta wa Kisumu pamoja na mama yake.
Katika moja ya mahojiano aliyofanya na mtangazaji Jimmy Kimmel, Lupita amsema umaarufu alionao hivi sasa nchini Kenya unaweza kuzidi wa baba yake ambaye ni seneta.
Vipande vya Movie aliyoifanya Lupita ya 12 Years a Slave
Vipande vya Movie aliyoifanya Lupita ya 12 Years a Slave
Source: Nairobi Wire



