Mwasiti Almasi amerudi tena na wimbo wenye ujumbe wa Mapenzi 'Serebuka'. Ni wimbo unaowapa moyo waliowahi kuumizwa na mapenzi kwa kutoa mfano wa wengi ambao walijitosa kwenye mapenzi na wakaumizwa. "Serebuka, unaweza pendwa tena.." Ni sehemu ya maelezo ya Mwasiti katika wimbo huu wake mpya wa Serebuka.
Wimbo huu umeandaliwa na Tudd Thomas utakufanya userebuke kimtondo na kuyasahau maumivu kwa muda kama wewe ni mmoja kati ya walioumizwa kimapenzi hivi karibuni.
Sikiliza hapa Chini..