NEWS

14 Januari 2014

PUB ya Aunty Ezekiel na Demonte yafungwa Chanzo Kiko hapa

Pub ya mwanadada Aunty Ezekiel iliyopo maeneo ya mwananyamala inasemekana imefungwa kutokana na kukosa management ya uhakika na pia kinachodaiwa kushindwa kwa Aunty Ezekiel kuiendesha Pub hiyo.


Kwa mujibu wa habari toka chanzo chetu kimoja cha habari kilichoshuhudia Pub hiyo ikiwa imefungwa kwa miezi kadhaa sasa zinasema kuwa chanzo kikubwa cha kufungwa kwa Pub hiyo ni gharama za vinywaji na wafanyakazi aliowaajiri zilikuwa juu na ndipo aunty akaona bora afunge kwa muda.

Tunamtafuta Aunty Ezekiel ili atueleze vizuri kuhusu kusimama kwa huduma katika Pub hiyo.