Lupita na Baba yake
Hatimaye mshindi huyo wa tuzo za Oscar ameumaliza mvutano huo kwa kutoa msimamo wake juu ya uraia wake.
“Mimi ni Mmexico na Mkenya kwa wakati mmoja” alisema Lupita. “Nimekuwa nikiona mvutano juu ya uraia wangu, lakini mimi ni Mkenya na Mmexico kwa wakati mmoja.”Alizungumza Lupita kwa mujibu wa El Mañana na kusisitiza tena “So again, I am Mexican-Kenyan and I am fascinated by carne asada tacos.”Lupita alizaliwa Mexico miaka 31 iliyopita lakini wazazi wake wote ni Wakenya, na baadae walirudi Kenya ambako alikulia hadi alipofikisha miaka 16, wazazi walipoamua kumrudisha Lupita Mexico ili akajifunze Spanish.
Alipoulizwa tuzo alizopata kama zinamilikiwa na Mexico, alisema “Tuzo ni za kwangu”.
News via:Niaje
