Kwa mujibu wa Nairobi Wire, Nazizi amesema kwa sasa bado yupo single.
“Nina marafiki wengi wa kiume, tunapiga picha kila mahali, hivyo ndivyo uhusiano wangu na marafiki zangu ulivyo”. Aliiambia Nairobi News.
Weekend iliyopita Sappy aliithibitisha kwa ushahidi wa picha pia kuwa yeye na Nazizi sasa ni wapenzi ambao wana mipango mikubwa juu ya uhusiano wao.
Aliongeza kuwa uhusiano wao ulianza kipindi cha Valentine ya mwaka huu Feb 14 na kuwa wanapendana kwa dhati.

Nazizi mwenye mtoto mmoja aliongeza kuwa hatashangaa kuona picha zingine zikitoka lakini akaendelea kusisitiza kuwa ana marafiki wengi wa kiume ambao yuko karibu nao.
“In fact, I won’t be surprised when more pictures come out. Like I said, I’m currently not seeing anyone, I just have many friends who are male and whom I am very close to.”

