Tovuti ya Page Six umeandika kuwa wapenzi hao wenye nguvu duniani wapo mbioni kutangaza ziara ya viwanjani ambapo watatumbuiza pamoja kwenye viwanja vikubwa 20 nchini Marekani. Wakati ambapo bado tarehe rasmi ya ziara hiyo haijatangazwa, inadaiwa kuwa inaweza kuanza June na huenda wakawa na show jijini New York, July 4.
Wawili hao wameliza ziara zao binafsi hivi karibuni ambapo Jay Z alimalizia ziara ya show 52 ya ‘Magna Carta…Holy Grail’ mwezi January, wakati Beyonce akimaliza yake ya ‘Mrs. Carter Show’ mwezi March.