Kanye West na Kim Kardashian wanajiandaa kufunga ndoa wiki chache zijazo jijini Paris, Ufaransa, lakini mgeni mmoja muhimu kwenye harusi hiyo hatokuwepo, rafiki wa Kanye, Jay Z. Jay Z alitosa ombi la Kanye kuwa mpambe wake wa harusi kwa sababu ambayo kwa wengi inaweza kuonekana nyepesi na ya kipuuzi. Hov hataki kuonekana kabisa kwenye show ya Keeping Up with the Kardashians!
“Of course, Kanye alimuomba Jay awe mpambe wake kwenye harusi. Lakini Jay alikaa ombi hilo,” mtu wa karibu ameuambia mtandao wa Hollywood life. “Jay hakutaka kuhusishwa kwenye reality show ya Kardashian. Kanye alimuambia Jay anaelewa kwanini amekataa, lakini bado aliumia sana.”
Ni wazi kuwa rafiki yako mliyefanya mambo mengi pamoja anapokutosa kwenye siku yako muhimu kama hiyo, ni lazima utaumia na ni ngumu kuelewa kwanini Jay kukataa hata kama alikuwa na sababu zake. Jay Z na Kanye West wameshirikiana kwenye album ya pamoja na wanajulikana jinsi walivyo karibu kwenye muziki.
Pia familia Kardashian lazima ichukulie kitendo hicho kwa shingo upande. Hiyo itamaanisha kuwa Jay Z haipendi familia hiyo au hajapenda Kim awe na mke wa rafiki yake Kanye.

