Mkali huyo wa Ten Over Ten liiambia radio AKBC ya Nigeria kuwa mwaka huu 2014 anatarajia kuachia albam yake ya tatu ambayo hata hivyo amesema hajaipa jina hadi sasa.
Mwaka 2008 aliachia albamu ya kwanza ‘You Know My P’ na mwaka 2011 alidondosha albam ya pili aliyoipa jina la ‘Super C Season’.
Rapper huyo pia amethibitisha kuwa anatarajia kupata mtoto wa pili na mkewe Nicole. Wana ndoa hao walipata mtoto wao wa kwanza wa kiume March mwaka jana walipokuwa Washington D.C.
