“Inaniuma kwasababu nikiwaangalia hao ni watoto wazuri sana na watoto wa mtu mkubwa sana lakini ambaye amepitia mambo mengi,” amesema. “Kwanza nina faraja kila ninapowaona japokuwa sina maelewano mazuri na wazazi wao kwasababu sijakuwa responsible kwa muda mrefu sana. Kwahiyo most of them wamekuwa wakiniona kama mhuni fulani ambaye amepoteza dira na msh*nzi fulani. Lakini nilikuwa nataka nifight nifanye muziki mkubwa nije kuwakomboa wao. Nimeweka nadhiri kwamba ‘Mwenyezi Mungu kabla hujanichukua mimi naomba nifanye kitu kidogo kwa hawa around ya mwisho then you can take me.”

“Na ndio maana kwenye kikao change cha kunegotiate peace na Clouds nilipresent kwamba mimi I got three kids I love them most na kama nisingeweza kuacha drugs sio kwasababu yenu ninyi mmesema, bali mimi kukaa chini na kuangalia kwamba kuna familia na watoto wananipenda. Wewe unaweza kunichukia lakini wanangu mwisho wa siku wao watahuzunika no matter the situation kwasababu damu ni damu. Narudi mara ya pili sababu I wanna be responsible for my kids.”
