The Jump Off ya 100.5 Times Fm ilipiga story na Joh Makini ambaye alieleza jinsi ambavyo kundi hilo linafanya kazi zake na jinsi ambavyo wanaweza kuzipangilia projects za solo artists na za kundi.
“Sisi hatuoni kitu cha kutuzuia yaani, tunasukuma vitu vyote at the same time, tunasukuma Crew na solo projects at the same time.” Alisema Joh Makini.
Alisema project yake na Nick wa Pili (Joh Makini Vs Nick wa Pili) inaendelea kurekodiwa na kwamba project hiyo inarekodiwa tofauti na projects za kundi au solo projects.
Msikilize hapa akieleza kwa undani kuhusu jinsi wanavyomshirikisha Bonta katika projects ingawa yuko mbali na ushirikiano wao na producers mbalimbali.