Katika hali isiyo ya kawaida, Elizabeth Michael aka Lulu amekana katu kutowahi kushirikishwa na wasanii hao na kwamba huenda umefanyika muujia.
Kupitia Instagram, Lulu ameandika:
“Mwe mwe mwe...!Mbona mnaninyasanyasa...'in Senga's voice'
I swear sina idea na Huku kushirikishwa....au kuna Elizabeth Michael'Lulu' mwingine!????
Dah...hebu mliosikia hyo nyimbo labda mniambieMana nashirikishwa ki miujiza jmn.”
Kwa maelezo ya Mapacha walipofanya interview na The Jump Off ya 100.5 Times Fm, wao walikuta mdundo wa wimbo huo studio ukiwa na sauti ya kike kwenye chorus na wakaipenda, baada ya kufanya kazi ndipo Tudd Thomas akawaambia kuwa sauti hiyo ameifanya Lulu.
So, Tudd aliwafunga kwenye gunia Mapacha?! Na Je, kwa nini Mapacha hawakumtafuta Lulu kumshukuru kwa chorus kabla ya kutangaza chochote?..Tunza majibu yako vizuri.
Mengine…endelea kusikiliza 100.5 Times Fm na kutembelea tovuti hii utayapata kiundani bila kupuuza neno.