NEWS

25 Juni 2014

Rick Ross akiweka pabaya kituo cha Hot 107.5, akana kuwekewa kizuizi na kundi la maadui

Rick Ross amekanusha taarifa zilozotolewa na muongozaji wa kituo cha Hot 107.5 kuwa aliwekewa kizuizi na maadui zake wakati akikaribia kuingia kwenye tamasha la Summer Jamz lililoandaliwa na kituo hicho cha radio, Jumamosi iliyopita.



Kituo hicho kiliwaambia mashabiki waliohudhuria tamasha hilo kuwa Rick Ross amewekewa kizuizi na watu na anahofia maisha yake na kwamba licha ya kumshawishi aingie Detroit alikataa na kuahirisha kuingia kwenye show hiyo.

Rapper huyo ameiambia TMZ kuwa huo ni uongo wa wazi, ukweli ni kwamba yeye alifika eneo hilo na akakuta geti limefungwa kwa hiyo hakuweza kabisa kuingia.

Amesisitiza kuwa hakuna mtu hata mmoja wa MMG au hata walinzi wake waliwahi kuzuiwa na watu wenye hasira au maadui wake.

Taarifa za kuwa alihofia uhai wake ni kama zilikuwa kichekesho kwa rapper huyo na kuuita uongo uliopitiliza.

Rick Ross aliwapa pole mashabiki wote waliohudhuria tamasha hilo kwa kupoteza masaa sita wakimsubiri bila mafanikio.

Taarifa hizi ni doa kwa HOT 107.5 hasa kwa matamasha mengine watakayoyaandaa.