
haswa pale katika ndoto za mtu akijaribu kukamilisha jambo fulani afike mahali anapotaka, hii imetokea kwa watu wengi sana, ila mmoja wapo ni huyu msanii Davido kutoka nchini Nigeria,ambaye kwa hivi sasa jina lake siyo lazima uingie google kumjua, kila mtu namfahamu fika kama King wa Skelewu.
Davido mwenyewe aliwahi kukiri kuwa hatosahau alichowahi kufanyiwa na Baba yake mzazi, kama walivyo wazazi wengi wa hapa Bongo, pale wanapoona mtoto ananza kujihusisha na maswala ya muziki, Davido yalimkuta hayo hayo,
Baba yake alikuwa anampinga vikali katika kujihusisha na maswala haya ya muziki, akiwa bado anatoka(underground) inasemekana kuwa, baba yake alikuwa anachukizwa na mambo aliyokuwa anayafanya na alikuwa hataki kabisa kusikia mambo ya kujihusisha na muziki, huku Davido kwa kujiamini aliendelea kufwata ndoto zake mwenyewe na kupita pingamizi hizo kutoka kwa baba yake mzazi.


