Kidole cha dereva kilichokatwa kwa risasi.
Tukio hilo la kinyama limetokea majira ya saa 7 na nusu jana mchana wakati sista huyo aliyekuwa na dereva wakitokea benki kufika eneo hilo kwa lengo la kununua mahitaji muhimu.
Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni dereva wa gari aliyefahamika kwa jina la Mark Patrick Mwarabu alisema kuwa marehemu alishangaa kuona amezungukwa na watu watatu waliokuwa wameshuka kwenye pikipiki aina ya Boxer na kumfuata kisha kumpiga risasi kadhaa.
Aliongeza kuwa, marehemu alikuwa ameenda kulipia pesa kwa ajili ya kununua mchele kwenye duka moja la nafaka kabla ya kuvamiwa na majambazi hao waliompiga risasi na kutokomea na mkoba wake huku wakimpiga risasi dereva huyo kidoleni.