NEWS

24 Juni 2014

Nicki Minaj aonesha mapenzi kwa Drake, 'that's my baby'

Nicki Minaj ameonesha upendo wake kwa member mwenzake wa YMCMB, Drake wakati anafanya mahojiano na Kojo na Jade wa kituo cha Capital Xtra, Jana.




Mwimbaji huyo ameeleza kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Drake anaependa kwa dhati kazi zake na kwamba amepanga kuingia nae studio hivi karibuni kurekodi wimbo utakaokuwa kwenye albam yake ya The Pink Print.

“I’m a massive fan of Drake, that’s my baby. And I hope and pray we’ll have a collaboration on there. I think that we’ll definitely have one on there.” Alisema Nick Minaj.

Nicki Minaj na Drake wamewahi kufanya kazi pamoja mara kadhaa na wameshirikiana kwenye nyimbo kama Moment 4 Life, Make Me Proud na Up All Night.