Bow wow ametangaza uamuzi huo kupitia Instagram akidai kuwa sasa ni wakati wa kuanza ukurasa mpya katika maisha yake.
Jina la Bow Wow litadumu kwa siku tano zilizobaki lakini baada ya tuzo za BET za mwaka huu (June 29), ataanza kufahamika rasmi kama Shad Moss.
“Baada ya tuzo za BET sitatumia tena jina la Bow Wow. Nitakuwa natumia jina langu halisi ‘Shad Moss’. Tumeweka historia kubwa kama Bow Wow. Sasa ni muda wa ukurasa mpya na changamoto.”Amesema Bow Wow.
“Bow wow haliendani na jinsi nilivyo leo, mimi ni baba, mfanyabiashara, mtangazaji wa TV, muigizaji na rapper! Ni muda wa MR. Moss kuchukua nafasi.” Aliongeza.