Rais Kenyatta ameyasema hao muda mfupi uliopita wakati akilihutubia taifa la Kenya baada ya mashambulio mawili yaliyotokea Mpeketoni juzi na jana.
Rais amewataja pia wanasiasa na baadhi ya maofisa kuhusika katika mashambulio hayo ambapo baadhi yao wameachishwa kazi tayari na watachukuliwa hatua kali ikiwemo kushitakiwa.
Kundi la Al Shabaab lilikiri kuhusika na shambulio la juzi usiku ambapo watu takribani 50 waliuawa.