Kuna bahati mbaya moja, ambayo baadhi ya wanawake hawaijui. Hii ni ile yakudhani kwamba, mwanaume akishaanzisha uhusiano na mwanamke au wakioana, kiwango cha kupendana kitakuwa ni kile kile milele.
Lakini ukweli ambao hawaujui ni kwamba, binadamu ana hisia na hisia hizi huweza kuchoka. watu wanapokaa pamoja au wanapokuwa pamoja katika uhusiano kwa muda mrefu, hufikia mahali ambapo kiwango cha hisia za upendo hushuka kwa maana kwamba, zimechoka.
Hebu fikiria inakuwaje ndugu au jamaa yako ambaye umekuwa ukitamani aje kukutembelea kutoka mbali anapokaa kwa muda fulani kwako, zile cheche za hamu zinapungua, wala bila kukosana au tatizo lolote?
Ni hisia zimechoka, hata unaponunua nguo au kiatu kizuri sana, baada ya kuda fulani, ule 'mchecheto' wa awali kukihusu,hupungua au kwisha. Ni suala la hisia pia, si kwamba, hiyo nguo au kiatu hukipendi tena. Kama mwanamke halijui jambo hili, linapotokea, hudhani kwamba, mwenzake sasa hampendi, na ndipo hapo kauli kama:
''Mwanaume akishakupata baada ya muda mfupi upendo wote wa awali huisha''
Haya ni malalamiko ya wanawake katika kujaribu kuonyesha ushahidi wa hali hii. wanashindwa kujua kwamba, kabla ya kuanzisha uhusiano au kuoana, hisia zilikuwa bado ziko juu, kwa sababu bado watu hawa walikuwa hawajaanza kuwa pamoja kwa muda mwingi
Ni mwongo anayeweza kusema kwamba, katika mahusiano yake au ndoa yake hajawahi kuhisi hisia za upendo kwa mwenzake kushuka angalau kidogo. kuna kutofautiana tu katika viwango vya kushuka kwa hisia hizo. lakini kila binadamu hisia zake za upendo hushuka.
Kuna sababu nyingi zenye kufanya kiwango cha hisia za upendo kushuka lakini kubwa huenda ni maumbile, sababu nyingine ni uwezo wa kila mmoja kubadilika kufuatana na mazingira, uwezo wa kutenda na kutoa kauli nzuri kwa mpenzi wake katika mahusino. lakini pia utayari kwa kila mmoja kuondoa zile tabia ambazo mwenzake anasema zinamkera.
Kushuka kwa hisia za upendo hakuna maana ya kuondoka kwa upendo. Upendo unapoondoka umeondoka, lakini hisia za upendo zinaposhuka zinaweza kurudishwa na hali ikarejea kama zamani tu. wakati mwingine hurudi zenyewe kama zilivyopotea.
Lakini wapo baadhi ya wanawake hisia za upendo za wenzi wao zinapopotea,hubabaika na kuharibu mambo