Nakaaya ameeleza kuwa hiyo ni sehemu ya mwanzo wa safari yake katika muziki wa hip hop bila kuacha uimbaji.
Amesema ngoma inayofuata itakuwa ya hip hop na amemshirikisha Mweusi G-Nako.
“Nimerekodi wimbo wangu utakaofuata unaitwa ‘Temana na Watu’ nimerap na nimemshirikisha G-Nako. Kwa hiyo ni kitu ambacho sasa hivi nakitest. Mwanzo nilikuwa naona haya sana. Unajua hip hop ni kitu ambacho watu wanakichukulia rahisi lakini nilikuwa bado sijapata confidence ya kuwa public nayo. Kwa sababu unaweza kuambia mara moja haya ‘hebu tupe verse’ kwa hiyo kama hujajipanga ndugu inakuwa inakula kwako.”