NEWS

30 Agosti 2014

Pata Michapo Ukweli wa Hussein Machozi kufumaniwa na mke wa mwanasiasa Kenya

Star wa bongo Hussein Machozi hatimaye amezungumzia tukio lililotokea mwezi uliopita na kupelekea vyombo vingi vya habari nchini Kenya kuripoti kuwa amekamatwa akizini na mke wa mwanasiasa maarufu mjini Mombasa, Kenya.

Hussein Machozi


Hussein Machozi alisema haya..

“Ukweli ni kwamba hiyo story imekuzwa yaani imekuwa kubwa sana tofauti na jinsi mambo yalivyokuwa. Kama masaa 24 nilipewa sasa mbona bado nipo Kenya…Ile ishu ilikuwa hivi, tulikuwa tumekwenda kuingia deal hotelini kama tunavyokutanaga, sasa Yule mtu aliyekuwa ananipa deal alikuwa yupo pale hotelini akaniita twende tukaongee kupanga mikakati na kila kitu, lakini baadae kumbe alikuwa na beef sijui na mume wake au sio bana, kwahiyo mume wake alikuja pale kuanza kumletea fujo lakini mimi sikuwa kwenye uhusiano wowote, watu wakaleta fujo pale na nini mimi mbona nikaondoka fresh tu lakini hamna lolote ni kwamba tulikuwa tumekaa nae tunaongea mchakato wa biashara…hotelini kama maeneo ya kupumzika hivi kama sehemu ya mikutano hivi”.